WAKATI mashindano ya u-miss yanaanzishwa Bongo, wazazi wengi walikuwa wazito kuwaruhusu watoto wao kushiriki wakiamini kwamba ni uhuni.
Kadiri miaka ilivyozidi kusonga mbele, taratibu walianza kuelewa kuwa siyo uhuni na wakawaruhusu watoto wao kwa kuyaona yana tija.
Matunda ya warembo yalionekana, lakini kumekuwa na dosari kwao, licha ya mafanikio makubwa wanayoyapata, asilimia kubwa hawaolewi.
Swali la kujiuliza hapa ni kwa nini hawaoleki, why?
Mwanasaikolojia mmoja aliwahi kusema, sababu inayosababisha warembo hawa wasiolewe au hata wakiolewa wasidumu kwenye ndoa ni jinsi wenyewe walivyojijenga akilini kuwa ni watu maarufu, wazuri hivyo wamekuwa wakichagua wanaume na kuishia kutumiwa, wakija kushtuka umri unakuwa umewatupa.