
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar, akiongea wakati wa hafla ya chakula cha jioni ilioandaliwa na taasisi hiyo kwa ajili ya kuchangisha fedha kufanikisha kampeni ya “Dawati kwa kila mtoto” inayoendeshwa na taasisi hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bank M, Bw.Nimrod Mkono(MB) akisikisiliza kwa makini kwenye hafla hiyo ambapo zaidi ya Shilingi Milioni 200 zilichangishwa kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya HMT Balozi Mwanaidi Maajar akiwa na baadhi ya viongozi wa Serikali kupakua chakula cha jioni kilichoandaliwa na taasisi hiyo.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar, Balozi Mwanaidi Sinare Maajar akiteta jambo na Waziri Mkuu Mstaafu ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Katiba Jaji Joseph Warioba, Dr. Salim Ahmed Salim pamoja na Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhan
