Usher Raymond IV amesherekea miaka 15 toka kuanzishwa kwa taasisi yake The New Look Foundation huko Atlanta Georgia, Mkali kutoka Atlanta Ludacris ndiye aliyesimamia mpango mzima, sherehe iliyohudhuriwa na watu 450. Mastaa waalikwa alikuepo director Kenny Leon, mwanamasumbwi maarufu Sugar Ray Leonard, muimbaji Rico Love, Josh Kauffman, producer mkali Jermaine Dupri, Blake Shelton na producer na muimbaji Bryan Michael Cox.
The President’s Circle Awards Luncheon ilifanyika pale katika hoteli ya St. Regis Atlanta, Usher alianzisha taasisi hiyo akiwa na umri wa miaka 20 akisaidiwa na mama yake.
Taasisi hiyo ilisherekea miaka hiyo 15 kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwashawishi vijana kupigania vitu wanavyovipenda katika maisha yao, Meya wa Atlanta Kasim Reed alipewa tuzo ya Service Legacy sambamba na watu wengine wakiwemo wadhamini na wanafunzi waliokuwa mstari wa mbele.
Taasisi hiyo ilichangiwa dola milioni 1 siku hiyo,mnada wa moja kwa moja ulifanyika wakati wa sherehe hiyo ambayo ilipanda na kufikia dola 98,000.
Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton, Muigizaji Robert De Niro na muimbaji Pharell Williams wote walipost video zenye ujumbe wa kumpongeza Usher Raymond kwa mafanikio ya Taasisi yake.
Taasisi ya Usher Raymond imesaidia zaidi ya watu 21,000 duniani kote toka kuanzishwa kwake mwaka 1999, Na lengo la taasisi hiyo ni kuwasaidia vijana kufikia malengo katika vipaji, elimu, na maisha na kutoa nafasi mbalimbali.