LEO NI SIKU YA FAMILIA DUNIANI, AMBAPO TANZANIA INAUNGANA NA MATAIFA MENGINE DUNIANI KUADHIMISHA SIKU HUYO, AMBAYO INAKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI IKIWEMO MABADILIKO YA KIJAMII, KIUCHUMI NA ONGEZEKO LA IDADI YA WATU , AMBAZO ZIMETAJWA KUA MIONGONI MWA SABABU ZINAZOSABABISHA KUVUNJIKA KWA MSHIKAMANO NA UMOJA WA NDANI YA FAMILIA NYINGI HAPA NCHINI
WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO BI SOPHIA SIMBA AMETAJA CHANGAMOTO HIZO KATIKA MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DAR ES SALAAM WAKATI WA KUELEZA SIKU HII YA KIMATAIFA INAYOADHIMISHWA IKIWA NA UJUMBE WA MWAKA HUU UNAOHAMASISHA MSHIKAMANO NA KUENDELEZA MAHUSIANO BORA YA FAMILIA NA MAKUNDI MBALIMBALI NDANI YA JAMII YAKIWEMO YA WATOTO, WAZEE WASIOJIWEZA , WAGOJWA, YATIMA AN WAJANE.
BI.SIMBA AMESEMA KUWA SEREKALI INAEDELEA KUWEKA MAZINGIRA MAZURI PALE INAPOWEZA KUHAKIKISHA KUWA MSHIKAMANO WA FAMILIA UNAIMARISHWA KWA KUTOA ELIMU NA KUOMBA MASHIRIKA YA KIRAIA, KIJAMII NA KIDINI KUUNGA MKONO SWALA HILO.