
Tee-Y Mix amezindua lebo yake ya muziki ambayo inaitwa Vivace Records inatamkwa Vi-Vah Chey Records. Tee – Y Mix ameshatengeza ngoma nyingi za mastaa wa Nigeria zilizohit sana kwa zaidi ya miaka 10 na kwa sasa amepiga hatua nyingine katika muziki wa town wa Kinigeria.
Tee Y
Akiongea katika uzinduzi Boss huyo wa Vivace Records Tee-Y Mix ameeleza kwamba upendo wake kwa muziki na jinsi anavyoona wasanii wengi wenye vipaji wakihangaika kufikia malengo yao katika soko la muziki wa Nigeria jambo lililochangia kuanzisha lebo yake ya Vivace Records.
Tee Y akiwa na wasanii Wake Waliosaini Katika Hiyo Lebo Yake
Akiwa mstari wa mbele kama mtayarishaji wa mapigo ya muziki, Tee-Y Mix ameona umuhimu wa kuinua vipaji ambavyo havijapata nafasi na vipo ndani ya Nigeria na anataka kusaidia kuibua mastaa wapya Wakinigeria.
Vivace Records inaanza na wasanii wawili wa Kinigeria mmoja naitwa Immaculate na Oyinkanade, wasanii wote wawili ambao anaanza nao ni wakali sana. Tee-Y Mix amesema muziki wa Nigeria hautatawala Afrika tu balihata majukwaa yote duniani.
