Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Bi. Usu Mallya akizungumzia uzinduzi wa ilani ya madai ya wanawake kwenye katika mpya iliyoandaliwa na mtandao huo kwa kushirikiana na wanaharakati wa masuala ya ukombozi wa wanawake, usawa wa kijinsia, haki za binadamu, demokrasia, utawala bora na maendeleo. Uzinduzi huo utafanyika katika viwanja vya TGNP siku ya Jumatano ya tarehe 08 mwezi huu kuanzia saa 4 asubuhi. Kushoto ni Mratibu wa Tanzania Women Cross Party Platform (TWCP) Dkt. Ave Maria Semakafu na kulia ni Lilian Mushi kutoka Jukwaa la Katiba Tanzania.
Amesema madai ya wanawake wa Tanzania katika katiba mpya ni mwafaka wa kitaifa unaotokana na mwendelezo wa harakati za raia na hususan za wanawake za kutaka mabadiliko ya msingi ya kimfumo, kisera na kisheria yatakayowezesha kukabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko makubwa ya mfumo wa uchumi wa dunia, mapinduzi ya technolojia ya mawasiliano na kuimarika kwa mifumo kandamizi.