Baada ya kuahirishwa kwa show za Mwana FA na ya Lady Jaydee zilizokuwa zifanyike May 31, show hizo tena zimepangwa kufanyika siku moja, June 14.
Mwana FA ambaye jina lake halisi ni Hamis Mwinjuma alitweet May 29 kueleza kuwa kama mazishi ya Mangwea yakifanyika mapema June 14 itakuwa ni siku ya show yake ya The Finest.
“Sina uhakika,but I’ll pick June 14th kama brother tutakuwa tushampumzisha,” alitweet FA. Na Jana usiku Mwana FA aliithibitishia Bongo5 kuwa show yake itafanyika June 14.
Taarifa ya tarehe mpya ya show ya Jaydee ilitajwa jana kwenye Twitter na yeye mwenyewe kwa kuandika:
“Long week end 13th June Mahakamani, 14th June Miaka 13 ya Jide. 15th June Bday ya Jide….it’s June, ni mwezi wangu. #Team Gemini/Anaconda.”