Soko la muziki Tanzania limekuwa kwa kiasi kikubwa, lakini pia ni soko ambalo lina ukosefu wa wasanii wa kike wakutosha tofauti na ilivyo kwa upande wa wanaume.
Dati ni msanii wa kike kutoka Tanzania ambaye anaishi nchini Sweden na kufanya shughuli zake za muziki nchini humo alipokwenda akiwa na umri wa miaka 19 tu.
Katika kuongeza idadi ya wasanii wa kike kwa sasa katika muziki ameibuka msanii wa kike ambaye anafanya vizuri kwa sasa na ngoma yake mpya inayoitwa “Can Do”.
Ngoma inayoitwa “Horray Horray” feat Nick B msanii kutoka Jamaica, ni ngoma ambayo ilifanya vizuri sana katika charts mbalimbali duniani, na ngoma iliyokuja kumtangaza vizuri zaidi na kuwa ngoma kubwa sana ni ngoma ya “Turn the Tables” ni ngoma ya mapenzi.
Kwa sasa Dati ameachia video ya ngoma yake mpya ya “Can Do” ambayo imefanyiwa nchini Sweden lakini video amefanyia Tanzania, Video ya “Can Do” ipo hewani katika vituo mbalimbali vya luninga.
Msanii ambaye Dati anamsikiliza na kumtazama sana ni Tracy Chapman.
Dati hayupo nyuma sana katika kutoa misaada kwa jamii, ameanzisha “Together We Stand Foundation” ambapo siku ya Jumanne 15 Desemba 2015 alitembea vituo vya vinavyolea watoto vya CHAKUAMA Sinza na Malaika Kids Kinondoni.