Kampuni ya Glitz imeandaa Toto Part kwa ajili ya watoto wa Dar Es Salaam na vitongoji vyake inayotarajiwa kufanyika Art Gallery Iliyopo Mbezi Beach siku ya Eid Mosi
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam muandaaji wa tamasha hili Dennis Ssebo alisema kwamba hii ni mara ya nne kuandaa TOTO PARTY kwa ajili ya watoto na wanatarajia kuanza kulipeleka tamasha hili na mikoani siku zijazo
Katika tamasha hilo watoto watapata nafasi ya kushiriki michezo mbali mbali kama vile Soka, Kuogelea, kusaka Hazina (Treasure Hunt) na kujipaka rangi usoni (Face Painting) na michezo mingine mingii huku wakikutana na marafiki wapya.
Aidha watoto watakao fika watapata nafasi ya kukutana na wenzao wanaoishi katika mazingira magumu ambao nao kupitia kampuni ya Glitz wamepewa nafasi ya kuja kusherehekea Skukuu
Mbali ya watoto kucheza katika michezo mbali mbali pia wazazi watakaowaleta hawata kaa bored kwani nao wameandaliwa michezo yao ya kikubwa kama kuvuta kamba ambapo washindi watazawadiwa zawadi mbali mbali.
Viingilio siku hiyo ya ni shilingi 3,000 kwa watoto na 7,000 kwa wakubwa
Nyote Mnakaribishwaa