Mkali wa mpira wa kikapu aliyestaafu na kuacha chata kwenye ulimwengu wa Mpira huo Michael Jordan amefunga pingu za maisha kwa mara ya pili. Staa huyo mwenye umri wa miaka 50 amefunga ndoa wikendi hii katika kanisa linaloitwa ‘Episcopal Church of Bethesda-by-the-Sea’ huko Florida na amemuoa mchumba wake Prieto mwenye umri wa miaka 35.
Ndoa hiyo iliyofungwa April 27 ilihudhuriwa na watu 300 wakiwemo mastaa wa mpira wa kikapu pamoja na wengine wengi walikuwemo mchezaji aliyekuwa nae Chicago Bulls Scottie Pippen na mastaa wengine wa NBA kama Patrick Ewing, Toni Kukkoc na Ron Harper. Mchezaji wa zamani wa mpira wa miguu Ahmad Rashad, na mkali wa Golf Tiger Woods, na muongozaji maarufu wa filamu Spike Lee.
Baada ya kutoka kanisani walihamia kwenye club maarufu ya kifahari ambayo iko karibu na nyumba anayomiliki Michael Jordan na hapo shangwe zikaendelea ambapo wasanii kadhaa walitumbuiza akiwemo Usher, K’Jon, na Robin Thicke.
Lakini badala ya zawadi za harusi, Michael Jordan aliomba waliohudhuria kuchangia taasisi ya James R. Jordan Foundation, na maua yalliyoletwa ‘wedding flowers’ yalitolewa kama mchango kwa Jupiter Medical Center.