Watu hao walioingilia mtandao huo wasiojulikana (Anonymous) ndio wamekiri kuwajibika na uvamizi wa account hiyo.
Msemaji wa jeshi amesema kuwa Meja Emmanuel Chirchir, hutumia akaunti yake ya Twitter kutoa taarifa kuhusu kundi la Al Shabaab.
Wavamizi hao walikosoa serikali ya Rais Uhuru Kenyatta wakisema kuwa inajali tu masilahi ya watu wenye ushawishi na haifanyi kazi ya kutosha kukabiliana na uwindaji haramu pamoja na dawa za kulevya.
Mwaka jana kikundi cha wavamizi wa mitandao wanaojiita Anonymous, walivamia mtandao wa wizara ya ulinzi ya Zimbabwe, na pia kuvamia mtandao wa chama tawala cha Afrika Kusini ANC.