
Prince George anaonyesha kwamba sasa anataka kutembea katika hiyo picha anayonekana hapo, picha hiyo ilipigwa mwezi Julai 2 na imetolewa na wazazi wake Prince William na Kate Julai 19 2014 ikiwa ni siku yake ya kuzaliwa akiwa anatimiza mwaka mmoja siku ya Jumanne.
Prince Geroge akiwa amevalia dungaree fupi na t-shirt ya bluu, amepigwa picha akionekana kujiamini kabisa akiwa amenyoosha mikono yake na macho yake yakiangalia mahali anapokwenda. Picha hiyo ilipigwa wiki chache zilizopita huko London kwa makumbusho yanayoitwa Natural History Museum ambako walimpeleka kutembea mtoto wao.
Ukiwa na watoto wewe mwenyewe huwezi kujua jinsi wanavyokuwa wakubwa haraka lakini watu wengine ndo wanaona, toka alipozaliwa mpaka sasa sio kichanga tena ni mtoto mkubwa tu sasa amebadilika.
George ambae ni watatu baada ya babu yake Prince Charles na baba yake Prince William, watakuwa Kensington Palce kwa ajili ya kushereka siku ya kuzaliwa George, wakiwa na watu wa karibu wa familia, na marafiki wa karibu wa familia hiyo.
