Mkali T.I King of South amesema yeye ndiye aliyemgundua demu ambae kwa sasa ni bad news kwenye gemu la Hip Hop duniani, Iggy Azalea ambae anatisha na ngoma yake yake ya ”Fancy” kutoka katika albamu yake ya “The New Classic” albamu iliyotoka mapema mwaka jana ikiwa imemtangaza vizuri na kupata mashabiki duniani kote. Iggy ni demu ambae anamnyima Nick Minaj usingizi kwa sasa.
Wakati akipiga stories na Big Boy Neighborhood kupitia kituo cha Power 106 T.I alisema ni mtu ambae alivutiwa sana jinsi Iggy Azalea alivyokuwa akianza na kumfanya aweze kukamata mashabiki wake.
“Nilijua kwamba kwa mipango mizuri iliyokuwepo hakuna kitu ambacho kingeweza kumzuia sky was the limit, Ana utofauti sana, sijali kama unanipenda au hunipendi nitafanikiwa tu, kwa hiyo unaweza ukaona sasa, hicho ndo kitu ambacho tunakiita umaarufu, huo ndo umaarufu, kwa wale wanaokubali wajibu wa kuangalia vipaji vipya na tunaona sasa, ni kazi yetu kugundua vipaji na kuviweka sehemu salama na hivyo kitu tulichukua muda kufanya sawa.” Alisema T.I
Alipoulizwa nini aliona kwa Iggy alisema:
“Tayari alishakuwa ametoa ngoma ambazo zilikuwa zikisumbua kwenye mitandao na watu wengi walikuwa wakiangalia, pia anamuonekana mzuri, Tulikaa nae tikiwa na Travis Scott na siku hiyo hiyo nah ii ilikuwa niliporudi nyumbani kwa mara ya pili, mara ya mwisho, Kweli najaribu kuitengeneza tena Grand Hustle kama Record label kama kitu katika kiwanda cha muziki, kwa hiyo natarajia vipaji vipya, kwa hiyo natafuta, Yo huyu msichana mzungu, sawa, mpe simu tuone lini tutakaa chini” alisema T.I
T.I tayari alishakuwa wanajuana na Iggy Azalea, Mwaka 2012, alianza kusaini na T.I kwenye label yake ya Grand Hustle records na kutoa album yake ya The new Classic chini ya label ya Imprint na Island records. T.I pia alitengeneza na kkushriki kwenye nyimbo zake nyingi.
Unajua Kuwa T.I Ndiye Alimgundua Iggy Azalea Demu Anayemnyima Usingizi Nick Minaj
Previous Story
Uingereza Yaporomoka Kisoka Duniani
Related Posts
-
-
Hivi Unajua Kuwa Ile Beats Ya Wimbo Wa Yahaya Wa Lady Jay Dee Ushawahi kupigwa Chini Na Msanii Mmoja Mkubwa Africa?
-
Kha! Hatimae Lupita Kadondokea Katika Penzi La Mwanamuziki Msomali K’Naam
-
Picha: Lady Jay Dee Nyumbani Lounge Re Launch
-
Maheeda Asema Rihanna Ndiye Aliyemuiga Sio Yeye Aliyemuiga Rihanna.
-
Kweli Pesa Wazimu, Hebu Ona Jinsi Nick Minaj Alivyomtam akiwa Natural Bila Mawigi Yake Ya Ajabu
-
T.I Na Tiny Wamjibu Flloyd Mayweather