
Mtangazaji mkongwe aliyewahi kutumikia RTD kipindi hicho sasa TBC, IPP MEDIA hatimae ABOOD MEDIA COMPANY Uncle J julius Nyaisanga Ameagwa Leo Katika viwanja vya leaders Club huku pakihudhuriwa na watu muhimu kutoka Serekalini akiwemo Makamu wa Rais Wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Dr.Gharib Bilal, Betty Mkwasa Mkuu wa wilaya ya Bahi, Mwenyekiti wa chadema na mkuu wa kambi ya upinzani bungeni Freeman Mbowe , Mkurugenzi wa makampuni ya IPP Media Bw, Reginald Mengi, Wanahabari kutoka vituo mbali mbali vya habari Tanzania, Wananchi Ndugu jamaa na marafiki

Makamu Wa Rais wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Dr, Gharib Bilal akitoa Salaam Za Rambi Rambi wakati wa kuuaga mwili wa Uncle J Julius Nyaisanga

Kutoka Kushoto Bwana Reginald Mengi, Makamu Wa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Gharib Bilal, Mkuu wa wilaya ya Bahi Betty Mkwasa, Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni Freeman Mbowe

Mwenye Shati Jeupe ni Abubakar Lyongo akiteta Jambo na Mtangazaji wa zamani wa Radio One ITV Misanya Bingi
Marehemu julius Nyaisanga anatarajia kuzikwa Kesho nyumbani kwao Tarime huko Mara
Marehemu Ameacha mjane na Watoto Watatu
Mungu ailaze roho ya Marehemu Julius nyaisanga Mahali pema peponi
AMEEN
