Baba Yake Chris Brown aeleza anavyoyachukia mapenzi ya mwanae na Rihanna anahofu mwisho wa yote huwa ni ‘Kifo’.Alitamani angekuwa na Jordin Sparks
Clinton Brown ambae ni baba mzazi wa Chris Brown amefunguka jinsi ambavyo hakuyapenda na hapendi kabisa uhusiano wa kimapenzi kati ya Rihanna na Mwanae. Na kama ingekuwa ile ya kibongobongo baba ananguvu ya kushawishi nani mwanae amuoe basi Rihanna ingekuwa ndo ishakula kwake kwa kura ya HAPANA.
Mzee Clinton Brown mwenye umri wa miaka 48 amefunguka katika interview na New York Daily News kuwa yeye binafsi asingependa kabisa Chris na RiRi warudiane tena. Alijaribu kutumia uzoefu na utu uzima kuzungumzia uhusiano huo ambao anaona sio kabisa.
“You have to have a balance in a relationship, you have to have someone who is spontaneous and whimsical but you also have to have someone who is grounded and logical.”
Huyu ndie baba yake mzazi Breezy aitwaye Clinton Brown
Alifunguka zaidi kuwa mapenzi kama haya huwa yanaishia pabaya sana, na hata akatoa mfano wa mastaa waliotangulia mbele ya haki na kusema mara nyingi mwisho wake hua ni kifo ama kuishia pabaya.
“sipendi kutumia mifano, lakini Michael Jackson, Whitney Houston na Amy Winehouse-I mean I cant go on and on. Hivi hii ni ipo tu kuwa hauwezi kuwa na bahati na umaarufu bila ‘kifo’ kuwa matokeo ya mwisho?” alijiuliza Clinton.
Japokuwa Clinton alimsifia Rihanna kwa uzuri na mafanikio lakini alitamani mwanae angekuwa na mtu mwingine lakini sio RiRi. Na kwamba alitamani kipindi kile angekuwa Jordin Sparks mshindi wa shindano la ‘American Idol’ aliyeimba na Chris Brown ‘No Air’ mwaka 2008, “binafsi nilimpenda Jordin Sparks alikuwa anajitosheleza msichana mdogo na mzuri sana.”
Alifunguka pia kuwa anafikiri Karruache Tran angefaa zaidi kuwa na Chris Brown kwa kuwa alikua na sifa zinazofaa, “Nilimpenda sana Karrueche . walionekana kuendana sana na kushibana. Muda wote alipokuwa karibu na mimi, alikuwa mkimya, mstaarabu, anataswira ya heshima na ndio picha aliyokuwa akionesha.” Alimzunguzia Karrueche aliyeachwa na Chris Brown na kuumizwa sana mwaka 2012 mwishoni.
Lakini mzee Clinton ambae aliachana na mama yake Chris Brown wakati Chris akiwa na umri wa miaka sita tu, sio kama hampendi Rihanna kabisa, kuna vitu anavipenda kwake ila akibadili tabia anaweza kuwa mama bora wa Chris. “ataweza kuwa mama bora baada ya kubadili tabia yake.”
Akamaliza kwa kuwa hadhani kama wataweza kuwa na mtoto wakiwa katika hali kama waliyokuwa nayo. Na kwamba haoni kitu kama hicho japo chochote kinawezekana pia.