Utaanzaje kufanya kufanya siku 3 kwa wiki kazi ya nani? Kama ni yako stress ndo hadi Jumapili unafanya kazi, unajituma zaidi ya kawaida, Imezoeleka kawaida mtu anafanya kazi Jumatatu hadi Ijumaa ambazi ni siku 5.
Lakini Mtu tajiri duniani anayefahamika kama Carlos Slim Helu ambae ni Mmexico aliyefanikiwa sana katika sekta ya mawasiliano anakadiriwa kuwa na kiasi cha dola bilioni 79.6, amewashauri watu wapumzike zaidi katika maisha ya kazi zao na kufanya kazi mara 3 tu kwa wiki badala ya mara 5 kama ilivyo kawaida.
Akiongea katika mkutano wa biashara huko Paruguay tajiri huyo mwenye miaka 74 alisema: “Watu wanatakiwa wafanye kazi kwa miaka mingi zaidi, mpaka kufikia miaka 70 – 745 na kufanya kazi mara 3 tu kwa wiki labda masaa 11 kwa siku, tutakuwa na muda mwingi wa kupumzika kwa ajili ya maisha bora, kuwa nasiku 4 za kumpizika itakuwa ni muhimu kuongeza shughuli za kiburudani na nji nyingine ya kujazwa na vitu vingine”
Je inawezekana?
Kama namuelewa Carlos unapopata muda mwingi wa kupumzika na kurelax hata akili na mwili unakuwa katika hali nzuri ambayo unapofanya kazi inakuwa katika ubora mkubwa tofauti na ukifanya kazi wakati haujapata muda wa kupumzika hata kazi unakuwa huipendi unafanya tu kukamilisha siku kwa sababu ni lazima, lakini ubora wa kazi unakuwa chini kwa sababu tu aliyefanya alikuwa amechoka na hapati muda wa kutosha kupumzika na kujiburudisha baada ya hapo ndo aende kazini.