Habari za kutatanisha zinazomhusu Peter Okoye wa kundi la muziki lenye mafanikio makubwa kutoka Nigeria P’Square zinasema kuwa msichana mmoja aitwaye Elshama Benson Igbanoi ambaye ni mpenzi wa siri wa Paul amejifungua mtoto wa kiume na
kudai kuwa ni wa staa huyo.
Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa Nigeria, Elshama mwenye miaka 19 alijifungua mtoto huyo wa kiume April 7, 2013 huko London Uingereza wakati girlfriend wa sasa wa Paul aitwaye Anita alijifungua mtoto wa Paul April 10, 2013 huko Atlanta Marekani, hivyo kumfanya mtoto wa Anita awe ni wa pili kwa Paul na si wa kwanza kama ilivyokuwa ikifahamika awali.
Chanzo kimesema Elshama aliyewahi kuwa miss alijifungua mtoto wa kiume katika hospitali ya Queen Charlotte and Chelsea Hospital iliyoko London Uingereza na kisha aliwasiliana na baba wa mtoto wake ambaye ni Paul ambaye hata hivyo alimkana mtoto na kumwambia ana mpango wa kwenda London kwaajili ya kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha kama kweli mtoto huyo ana damu yake.
Elishama alisema hajawahi kufanya mapenzi na mwanaume mwingine na amekuwa mwaminifu kwa Paul toka alipomtoa bikra akiwa na miaka 17.
Story cr:Bongo 5