Akiongea na gazeti Nigeria, Olori super girl, Victoria Kimani alieleza kitu kibwa kilicho miongoni mwa jamii katika kiwanda cha burudani kwamba wanawake wengi hawaheshimu na wanapokea mashambulizi mabaya wakati tayari wanafanya juhudi kwa kufanya kazi sana ili wawe na mafanikio.
Alitaja mawazo yaliyoenea kwa sasa kwamba wanawake lazima ajiamini ili akubalike, anasema mwanamke kupata mafanikio sio lazima awe Malaya.
“Kuwa msanii wa kike haimaanishi kwamba nafanya kazi bure, eti kwa sababu nawaimbia tu nikiwa nimevaa nguo nzuri kwenye jukwaa na kwenye TV, hainifanyi niwe Malaya, nafanya kazi sana” aliongeza Victoria Kimani.
Alisema pia kuna hukumu nyingi sana juu yao, unafiki, vitisho kwamba wanawake wengi wasanii wa Afrika Mashariki wanajihusisha na umalaya.