Ni picha ya kujipiga mwenyewe maarufu kama SELFIE ya Star wa TV Ellen Degeneres aliyoipiga wakati wa Tuzo za Oscar Jana inasemwa kuvunja rekodi katika mtandao wa tweeter tangu kuanzishwa kwakwe ikiwa ime retwetiwa mara nyingi zaidi na kuizidi ile ya Raisi Wa Marekani barak Obama Aliyojipiga akiwa na mkewe wakati aliposhinda Urais.
waliotokea katika picha hiyo ni pamoja na mshindi wa Kipengele cha muigizaji mwanamke msaidizi Lupita Nyong’o kutoka Africa, Kaka yake Lupita, Brad pitt, angelina jolly, Julia Roberts, Kevin Spacey,Bradley Cooper, Merly Streep, Jeniffer Lawrence na wengine kibao