Mafanikio yeyote hayaji bila juhudi na maarifa uvumilivu na kuamini huku ukiwa na uthububu
Ndivyo ilivyo tokea pia kwa msichana lupita Nyong’o,
haikuwa rahisi kama tulivyofikiria, hakutokea tu hapo alipo kama tunavyomuona ameanzia mbali akijitahidi na kujitahidi
baada ya kufanya filamu nyingi akiwa nchini kwao Kenya, akapata nafasi ya kuigiza katika hiyo filamu ya ’12 years a slave’ alipata wasawasa kwa maana alikua na mwaka mmoja wa kufanya jambo kubwa kabla hajaendelea kuishi marekani, anasema haikuwa rahisi, haikuwa rahisi kutokana na ugumu wa ma director kutamka jina lake, LUPITA NYONG’O, lakini pia rangi yake ilionekana kikwazo katika hatua za awali muonekano na hata umbo lake,
Aliogopa kidogo na kupata wasiwasi lakini si vitu vilivyomfanya akate tamaa kamwe, Aliendelea kuchapa kazi na kuamini katika ndoto na mafanikio yake anasema kijana mmoja aliyewahi kufanya nae Movie moja huko nchini Kenya, lakini pia kijana huyo alimuelezea ya kuwa hata baada ya kufanya 12 years a slave alikuwa Kenya na hakuwa na imani kubwa ya kufanya vizuri kutokana na changamoto nilizozitaja hapo awali ilimbidi wakati huo afikirie kufanya jambo lingine kama asingefanya Vizuri katika filamu hiyo ili aendelee kubaki Marekani,
Kijana huyo alimuelezea pia lupita si mtu aliyekuwa anafanya uigizaji ili apate umaarufu la hasha Lupita alifanya uigizaji maisha yake ndiomaana hata wao walipohitaji kwenda Club baada ya kazi yeye alirudi nyumbani kuendelea kupitia Script yake ya siku itakayofuata
Anasema kijana huyo Lupita Anastahili Tuzo Hiyo Ya Oscar aliyoipata Usiku wa kuamkia Jumapili katika kipengele cha Muigizaji Bora Mshiriki kwa wanawake
Rais Wa Kenya Uhuru Kenyata Ni Miongoni mwa watu muhimu waliomtumia salam za pongezi Lupita Nyong’o na kuelezea kufurahishwa na kwa jinsi anavyojivunia yeye.
Lupita Anasema ” NO MATTER WHERE YOU COME FROM, YOUR DREAMS ARE VALID”