
Kwa zaidi ya wiki moja iliyopita habari zilisambaa kwamba binti Mtanzania aliekamatwa na dawa za kulevya nchini Misri angenyongwa siku za karibuni kutokana na hizo dawa alizokamatwa nazo.
Baadae balozi wa Tanzania Egypt alijitokeza na kukanusha taarifa za kunyongwa na akakubali kwamba kweli kuna Watanzania wawili wamekamatwa ambao ni huyo msichana na ndugu yake wa kiume ambao ni wakazi wa Magomeni Dar es salaam na kwamba wanashikiliwa na polisi huku wakisubiri kesi yao.
pata kuona video ya mahojiano ya TV na msichana huyu ambae anadai alikwenda Misri kumtafuta binamu yake, begi alilokamatwa nalo ni lake ila alikua hajui kama lina dawa za kulevya.
Video inaanza na kiarabu baadae anahojiwa kwa kiingereza…

1 Comment
video ya binti wa unga haifunguki