ile video iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu sana ya Yahaya ya Lady Jay Dee Inatarajia kuzinduliwa Kesho Ijumaa Tarehe 16, katika kiota cha burudani cha nyumbani lounge morocco jijni dar.
Jay dee ameandika kupitia Blog yake kuwa :
‘Hivi sasa iko tayari, tumeona si vibaya tukaifanyia kiji party kidogo cha utambulisho
Kikiambatana na BBQ, na Shooters za hapa na pale kuupendezesha usiku wako.
Party ya kuitambulisha Video ya Yahaya, ambayo imefanywa na Ogopa DeeJays
Itaanza saa 4:00usiku (10:00pm) ikiambatana na burudani ya muziki toka kwa JayDee na Machozi Band’
Msanii Dude kutoka bongo Movioe ndio aliyeigiza kama muhusika Yahaya Aliyetajwa katika mwimbo huo