Msichana mdogo Yatima wa kituo cha kulelea watoto ya waishio katika mazingira magumu huko nchini Thailand amefanya maamuzi magumu baada ya kumkatalia Reality Tv Star Kim Kardashian Offer ya kumuasili (adopt) ili kumbadilishia maisha yake badala yake ametaka kubaki nchi kwao na kuendelea na maisha pamoja na wenzake walioishi nao katika kituo hicho kwa muda mrefu msichana huyo mdogo wa umri wa miaka 13 tu ambaye anaitwa pink alisema alipatwa na mshtuko baada ya Kuona Milionea huyo Amevutiwa nae na kwamba anataka Kumuasili lakini badala yake binti huyo alitaka kubaki Thailand na kusoma huko huko ili aweze kuwasaidia watu wake wanaoishi katika mazingira magumu na mayatima aliokuwa nao. Binti Huyo aliteka hisia za kim Kardashian mara baada ya kutembelea kituo hicho kinachojulikana kama Thailand’s Phang Nga
Prividence ambapo mkoa hilo watu 4000 walipoteza maisha kwa tukio la kimbunga cha Tsunami mwaka 2004 Pink Ambaye ni mwanafunzi bora kituoni hapo alipelekwa na mama yake katika kituo hicho kwasababu ya hali ngumu ya umasikini ili aweze kujipatia elimu yake.. Alizawadiwa bangili ya mkononi na Star Huyo mpenda kukaa uchi mwezi wa nne alipofika hapo kutengeneza kipindi chake cha Keeping Up With Kardashian Lakini baada ya kuambiwa kuwa sasa Kim angetaka kumuasili pink alisema “Kila mtu anapenda kuwa na maisha ya tofauti au maisha mazuri zaidi, Me Pia, Lakini baada ya kutafakari Zaidi nikaona halitakuwa jambo la busara kwangu, Kwasababu naona nitainshi tofauti sana , sikuwa tayari kwa jilo” alimalizia Pink