
Mnaijeria Obabiyi Aishah Ajibola Ametwaa Taji la mrembo wa dunia wa kiislam, mashindano yaliofanyika jana sep 18 Mjini Jakarta Indonesia ambapo majaji sio tu kwamba walikua wanaangalia uzuri wa wasichana hao na maumbo bali uelwewa wa dini ya kiislama na namna warembo hao walivyoweza kukariri aya katika kitabu Kitukufu cha Quraan Obabiyi Aishah Ajibola, 21, alisujudu ikiwa ni ishara ya kumshukuru mungu mara baada ya kutajwa kuwa mshindi wa taji hilo kwa mwaka huu katika shindano hilo ambalo lina miaka mitati sasa tangu kuanzishwa kwakwe Mshindi huyo alipata zawadi ya fedha taslim 25 million rupiah (£1,375) na trips ya kwenda Mecca na India. mashindano ya dunia ya kawaida yatafanyika katika kisiwa cha Bali huko huko Indonesia baada ya kuhamishwa Jakatra yalipokua yafanyike baada ya maandamano yaliyotokea kupinga mashindano hayo kutokana na nchi hiyo kuendeshwa kwa misingi ya dini ya kiislam
