Mahakama ya juu nchini Kenya hii leo inatarajiwa kutoa uamuzi wake juu ya kesi iliowasilishwa kwake na muungano wa CORD, inayotiliashaka matokeo ya uchaguzi uliomalizika hivi majuzi, uliompa ushindi Uhuru Kenyatta na kutangazwa kama rais mteule wa Kenya.
Uamuzi huo unatizamwa kama mtihani kwa mfumo wa demokrasia ya nchi hiyo, miaka mitano baada ya ghasia za baada ya uchaguzi kusababisha vifo vya takriban watu 1200.
Hata hivyo rais anayeondoka madarakani Mwai Kibaki amewaomba watu kuwa watulivu wakati wakisubiri uamuzi huo utakaomuunga mkono Kenyatta kama rais wa 4 wa Kenya au kuwarudisha tena wakenya kupiga kura kwa mara ya pili.
Kiongozi wa muungano wa CORD Raila Odinga amesema uchaguzi uliofanyika Machi 4 ulikumbwa na udanganyifu wa hali ya juu.