Jeneza la aliyekua Rais wa Venezuela Marehemu Hugo Chavez, limepelekwa kwenye chuo cha Kijeshi ambapo litabakia kwa muda wa siku tatu ili kutoa fursa kwa waombolezaji kutoa heshima za mwisho.
Tayari baadhi ya viongozi wa juu wametoa heshima zao za mwisho kwa marehemu Chavez sambamba na wanafamilia akiwemo mama mzazi wa Chavez, Bibi Elena, watoto wake watatu wa kike na mtoto mmoja wa kiume.
Msafara wa kupeleka mwili wa marehemu Rais Chavez kwenye chuo hicho cha kijeshi uliongozwa na makamu wa Rais, Nicolas Maduro na Rais wa Bolivia, Evo Motales.