Wasichana wawili ambao ni ndugu mmoja akiwa na umri wa miaka 14 na mwingine miaka 15 wamekutwa wamekufa kwa kuning’inizwa mtini
Polisi wamesema Wasichana hao wadogo wanaotokea katika jamii ya kawaida vijijini walipotea ghafla mara baada ya kutoka kwenda maliwatoni huko kijijini kwao Uttar Pradesh may 27
kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters wasichana hao walikutwa wametundikwa katika mti wa muembe baada ya kubakwa na wanaume watano
Hata hivyo polisi wamemkamata mtuhumiwa mmoja wa tukio hilo huku wakiwatafuta wengine wanne
polisi wamesema Uchunguzi umeonyesha wasichana hao walibakwa kisha kuu wawa ku kunyongwa mtini