Watetezi wa haki za binadamu na taasisi za habari nchini wameitaka serikali kuyafungulia magazeti ya mwananchi na Mtanzania mara moja kwani kitendo cha kuyafungia magazeti hayo kimekiuka ibara ya 18 ya katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.
Serikali kwa kuyafungia magazeti hayo moja kwa moja kumeondoa haki ya kupata habari lakini pia ni ukiukwaji wa haki za binadamu kwani athari zake zinawagusa pia wafanyakazi wake ambao watakosa ajira katika kipindi chote cha utekelezwaji wa adhabu hiyo.
Akizungumza kwa niaba ya watetezi hao, mratibu mkuu wa mtandao wa watetezi wa haki za binadamu (THRDC) Onesmo olengulumwa amezitaka asasi za kiraia na taasisi za habari kuongeza nguvu katika kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na kampuni ya Hali Halisi Publishers dhidi ya kufutwa kwa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 ambayo ameitaja kuwa ni kandamizi na inapingana na katiba ya Jamhuri ya Muungano na sheria za kimataifa.
Hatua ya kuyafungia magazeti ya matnzania na mwananchi inafanya idadi ya magazeti yaliyungiwa mpaka sasa kufikia matatu ikiwemo gazeti la mwanahalisi ambalo lilifungiwa kwa muda usiojulikana. —