
Makaziwe Mandela
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, Wanawe rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, wameamua kuchukua hatua za kuwaondoa wasaidizi wake watatu kutoka katika makampuni anayoyamiliki.
Makaziwe na Zenani Mandela wanadai kuwa watatu hao hawana haki ya kuwa kwenye bodi mbili za kampuni hiyo ambazo ni za thamani ya dola milioni 1.1
Zenani Mandela
Kesi hiyo inakuja wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu afya ya Mandela mwenye umri wa miaka 94
Mandela aliondoka hospitalini baada ya kutibiwa ugonjwa wa mapafu pamoja na homa ya mapafu, na katika rekodi amelazwa hospitalini mara ya nne katika kipindi cha miaka miwili.
Duru zinasema kuwa kumekuwa na mzozo wa kichinichini tangu mwaka 2005 wa kudhibiti pesa zinazotokana na mauzo kwenye jina la Mandela hususan picha alizokuwa anachora akiwa jela.
story credit sammisago.com
