Wamekuwa watoto waliokamata headlines na kuweka historia, Curtis Fairchild Jones (13) na dada yake mwenye umri wa miaka 13, Catherine, walikubali kwamba walimuua mpenzi wa baba yao anayeitwa Sonya Nicole Speights mwenye umri wa miaka 29, mwaka 1999. Dalili za mwanzo zilionyesha mauaji yalisababishwa na wivu, lakini baada ya mafaili na ripoti kuangaliwa vizuri ikagundulika aliyetakiwa kuuawa alikuwa Speights, baba yao na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akiishi nao, ambaye wanamlalamikia alikuwa akiwanyanyasa kimapenzi.
Mpango wao ulikuwa kuwaua wote watatu.
Siku chache baada ya shirika linalojulikana kama Department of Children and Families lilikubali dalili za watoto hao kunyanyaswa kimapenzi lakini walifunga upelelezi, Catherine alikuwa akioga akasikia mlango wa bafuni unafunguliwa. Mtu aliingia kumchungulia, Akawa anajichua (Masturbate), akiwa anatetemeka, akiwa kwenye kona ya bathtub akilia, alisema Catherine.
Baadae usiku ule, alifanya maamuzi yake akasema “Nakwenda kuua kila mtu”
Kutokana na mahojiano na makaratasi ya mahakama, Catherine alimwambia Curtis kuhusu mpango wake, Catherine akamwambia atamsaidia, Watatumia bastola 9mm semi-automatic ambayo baba yao aliificha chumbani.
Lakini kila kitu kilienda kinyume baada ya kumshoot Speights pekee yake, kwa uoga wakakimbilia kwenye mbao karibu na nyumba yao St. John, Fla…wakajificha hapo mpaka polisi walipowakamata asubuhi Januari 7, 1999.Wakawa watoto wadogo kabisa katika historia ya Marekani kuhukumiwa kama watu wazima kwa kesi ya mauaji. Wakahukumiwa kwenda jela miaka 18, na wakitoka watakuwa chini ya uangalizi maisha yao yote.
Kabla ya kutoka nje ya mahakama, Curtis alimgeukia hakimu, Tony Hernandez na kumuuliza kama angeweza kwenda na Nintendo video game yake jela. Jibu unalo? Jela ni sehemu ambayo unakosa vile vitu unavyovipenda ili ujifunze ulichofanya sio sawa ndio maana upo hapo.
Muda Wa Kuwa Huru Unakuja
Kwa sasa Curtis ana tattoo mbili, amechora panther kwenye mkono wake wa kushoto na neno “Mob” kwenye tumbo lake. Curtis Jones anatoka jela akiwa amezoea jela akiwa na ufahamu mdogo wa uraiani. Pia anaishi na mzigo mkubwa, akitakiwa kuangaliwa maisha yake yote, kitu ambacho mwanasheria mmoja alielezea kama ni sawa na mguu mmoja umeganyaga ganda la ndizi na mguu wa pili katika idara ya kurekebishwa tabia. Curtis Jones anaweza kutoka mwezi mwishoni wa Julai na na dada yeke Catherine anaweza kutoka mwishoni wa Agosti.
Kuwa chini ya uangalizi inamaana kwamba wako hatarini kurudi jela tena kwa kosa lingine lolote ambalo wamekubaliana hawatafanya watakapokuwa huru.
Wakiwa nje watatakiwa walipe dola 50 kila mwezi kulipia gharama za wasimamizi baada ya miezi 18, kutotumia kilevi chochote kupitiliza, kutokwenda sehemu yeyote bila ushauri kutoka kwa waangalizi wao. Wanaweza wakapata mwanasheria kubadilisha masharti waliyowekewa wakiwa nje au waombe ifutwe kabisa baada ya muda fulani.
Sio Curtis sio Catherine, wamechagua kutoongea na vyombo vya habari, Profesa wa Paolo Annino wa Florida State University law, ambaye aliwahangaikia wasamehewe, alisema Curtis amemuomba asiseme chochote kuhusiana na mambo yake.
Catherine, ambaye alipata mpenzi na kuoana kupitia rafiki wa kalamu (Pen Pal) anategemea kutoka mwezi ujao.
Alivyoonja Ladha ya Uhuru na kurudu ndani
Curtis Jones alipata ladha ya uhuru kidogo baada ya Hurricane France kupiga na kuangusha fence, alikamatwa saa 24 baadae na akaongezewa siku 318 katika kifungo chake, zaidi ya hilo hajawahi kuishi mwenyewe.
Ukilinganisha akili za watu waliopo nje ni tofauti sana, watu waliopo nje wanafanya vitu bila heshima, lakini ukiwa jela ni tofauti.
Wafungwa wakiwa jela huwa na heshima, na ukiwa na heshima inakuwa ni rahisi kutoka kwa sababu unaonekana kwamba umejifunza na umekuwa mtu mzuri, na hivyo pia ndivyo unavyotakiwa uwe kutokana na mamla ukiwa mtukutu kwanza ndo mateso yanazidi.
Unampa ushauri gani mtu aliyekulia jela, ametumia muda mwingi wa maisha yake akiwa na wahalifu na ambaye anajua kidogo kuhusu dunia?
Mimi namshauri akae mbali na bars, asilewe, kikubwa achukue vitu taratibu, aende taratibu asikurupukie vitu taratibu atazoea la sivyo anaweza kurudi jela, na hilo sio kosa lake ni kosa la akili yake, kwa sababu hapa akili inahusika sana, anahitaji maelekezo ya hali ya juu