Lori la mafuta limeanguka katika eneo la milima ya sekenke mkoani singida na kuua watu wanne hapohapo.
Chanzo cha ajali hiyo ni breki kufeli kukamata wakati lori hilo lilipokuwa linashuka mlima huo.
Shuhda wa ajali hiyo amesema kwamba Lori hilo lilipoacha njia lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea kuongea shuhda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kwa moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea.