Familia moja nchini china imejikuta katika wakati mgumu wa kutafuta haki ya kumuua binti yao mwenye umri wa miaka 4 anayesumbuliwa na kansa ya jicho.
Wazazi hao ambao ni wakazi wa jimbo la Shaanx Province nchini China waligundua kansa hiyo iliyokuwa ikimsumbua binti yao miaka miwili iliyopita na walihangaika katika hospitali nyingi kwa lengo la kumpatia matibabu binti huyo lakini madaktari waliwahakikishia kuwa ugonjwa huo hauwezi kupona.
Licha ya madaktari kuondoa jicho la kushoto la binti huyo kwa njia ya upasuaji lakini kansa hiyo iliendelea kusambaa kwa kasi na sasa imeanza kushambulia shavu la binti huyo hali iliyopelekea wazazi hao kudai haki ya kisheria ya kumaliza uhai wa binti yao huo.
Baba wa binti huyo alinukuliwa akisema “Tunatumaini kuwa tutapata hospitali itakayotusaidia kumpunguzia binti yetu maumivu haya makali aliyonayo pamoja na kumuondoa kwa amani hapa duniani”
Kwa mujibu wa sheria za sasa nchini China ni marufuku kukatisha maisha ya mgonjwa hata kama ni mahututi kiasi gani.