Wazazi wa mtoto Ashya King aliyetoroshwa kutoka wodini alikokuwa akiuguzwa kutokana na uvimbe uliotokana na ugonjwa wa kansa ya ubongo mjini Hampshire Uingereza wamekamatwa mjini Madrid nchini Hispania baada ya kumuamishia mtoto wao huyo mwenye umri wa miaka 5 katika hospitali ya watoto ya Malaga ambapo hali yake ya kiafya inasemekana kuimarika.
Hakimu wa jijini Madrid alisema anafikiria kuwaweka ndani kwa muda wa masaa 72 wakati akifikiria ombi lililotolewa na serikali ya uingereza ya kuwakabidhi wazazi hao kwa polisi wa uingereza.
Kumekuwa na wito kutoka kwa watu mbalimbali wakitaka wazazi hao waruhusiwe kuwa na mtoto wao katika kipindi hiki kigumu kwa mtoto huyo huku naibu waziri mkuu wa uingereza alisema kuwa haikuwa sahihi kutumia nguvu kubwa dhidi ya wazazi hao waliodai kuwa lengo lao la kumuhamisha mtoto huyo lilikuwa ni kupata huduma bora kwa ajili yake.