Muigazaji wa filamu wa nchini Marekani Wesley Snipers ameachiwa huru kutoka kifungoni baada ya kutumikia adhabu ya kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kukwepa kulipa marejesho ya kodi.
Muigizaji huyo alikutwa na makosa ya hayo mwaka 2008 baada ya waendesha mashitaka kusema kuwa alishindwa kulipa marejesho hayo ya kodi kwa takribani muongo mmoja na kujipatilia mamilioni ya dola.
Snipes mwenye umri wa miaka 50 ni mmoja wa kundi la watu waliokuwa wakikosoa uhalali wa sera ya serikali ya Marekani katika kukusanya mapato.
Staa huyo wa filamu za ‘Blade’ alikata rufaa katika mahakama ya Atlanta kupinga mashitaka yake akidai kutotendewa haki.Hata hivyo alijikuta akihukumiwa na kuingia katika gereza la McKean federal huko Pennsylvania mwaka 2010.
Kufuatia kuachiwa kwake, msemaji wa gereza la kurekebisha tabia amesema ataendelea kuwa chini ya uangalizi wa Ofisi ya New York ya Urekebishaji tabia kwa jamii hadi mwezi Julai 19 mwaka huu.