Haijathibitishwa Bado lakini mpaka sasa hapajatokea Rekodi Nchini uingereza Ya Mwanamke mwenye tumbo kubwa la ujauzito kama mwanamke huyu alikua na na ukubwa wa inch-55
Mwanamke Huyo mwenye miaka 29 Lara Carpenter-Meck aliongezeka uzito na ukubwa wa tumbo lakiasi kutotoshea katika nguo za kawadia za mama mja mzito
“Katika wiki ya 12 tu watu wakaanza kuniuliza na kushangaa ukubwa wa mimba yangu, Na tumbo langu likawa linaendelea tu kukua kwa kasi ya ajabu nikajishangaa Tumbo langu likikua kwa kasi ya ajabu, ilikuwa ni mimba yangu ya kwanza hivyo sikuwa najua nini kinatakiwa kiwe next but niligundua tu ukuaji huu wa tumbo haukuwa wa kawaida hasa kutokana na kuwa na mtoto mmoja tumboni” alielezea mwanamke huyo
Katiki wizi ya 32 wauguzi walimueleza lara kuwa mtoto wake ametimiza uzito wa 6lbs, uzito unaotajwa kuwa na mtoto aliyetimiza miezi tisa tayari
Hata hivyo baada ya wiki nne zilizofuata Lara alienda kwa ajili ya kujifungua baada ya chupa kuvunjika bila kutarajiwa
Lara na partner wake wamemkaribisha mtoto wao waliompa jina la Savannah, Aliyezaliwa na kilo 9lbs 5oz
“Chris na mimi siku zote tulidhani tungepata mtoto wa kiume kutokana na ukubwa wa tumbo langu , Basi ikawa ni mshangao mkubwa sana baada ya kuja kujua ni kichanga cha kike, alikuwa ni kaschana kakubwa na kazito” alisema Lara
“Tumekuwa na Furaha kupata mtoto wetu wa kike akiwa na afya nzuri kabisa, ilibidi tukubaliane na hali kuwa kimekuwa kiumbe kikubwa tangu kikiwa ndani” Lara alisema