Muda mfupi tu baada ya Chriss Brown kumaliza show yake kwenye after party ya YMCMB Drake na Lil Wayne kwenye club ya Supperclub huko Hollywood, kuna watu ambao walianza kupigana na mmoja wao alichomwa kisu. Na mtu huyo aliyechomwa kisu alipelekwa hospitali na alitegemewa kuwa atakuwa fresh.
Vyombo vya dola vinaripoti kwamba hawakumkamata mtu yeyote kwa sababu hakuna mtu yeyote alitoa taarifa yeyote ambayo ilipelekea kutokea tukio hilo. Polisi mmoja amesema wanaamini hii yote ni kuhusu mtu anayekuwa na Chriss Brown sehemu mbalimbali wanazokwenda, mwisho wa siku mtu amevuja damu.
Taarifa zimesema kwama Loa Angeles Police Department kisiri wamekutana na wamiliki wa wa club hiyo wakiwalazimisha kutaja watu waliokuwa na Chriss Brown, lakini club hiyo inatengeneza pesa nyingi kupitia wao kwa hiyo wanawaruhusu wanaingia na silaha.
Mtu mmoja kutoka vyombo vya sheria amesema wakati Chriss Brown na watu wake wanapotokea, huwa wanajua nini kinafuata, huwa vichwa vinawauma.
Chriss Brown ajahusishwa na tukio hilo la mtu kuchomwa kisu lakini plisi wanasema wanajua yote haya yameanzia kwa Chriss Brown na wenzake.
Hapa unakumbuka watu watatu walipigwa risasi akiwemo Suge Knight, wakati Chriss Brown alipokuwa akipiga show katika club ya 1OAK mwezi uliopita.
Jana katika Under cover stories kama unakumbuka kulikuwa na stori ya Chriss Brown akisema kwamba amebadilika sana amekuwa hafanyi tena mambo ya kijinga, na ni baada ya kutoka jela alisema amebadilika na video za ngoma kwenye albamu ya X ataonyesha jinsi alivyokuwa.
Ila kwa hili lililotokea mtu akachomwa kisu inaashiria nini? Bado anaendelea na mambo yake, lakini hakuna ushahidi kama yeye au wenzake walihusika ila polisi wanamashaka kwamba mpaka mtu anachomwa kisu imeanzia kwa Chriss Brown na wenzake.