Yule Mkalimani wa lugha za ishara Thamsanqa Jantjie aliye ushangaza ulimwengu wakati wa ibada ya Aliyekuwa Rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini Nelson Mandela amelazwa katika Hospital Ya wagojwa wa akili
Mke wake Siziwe ameseama huenda mumewe ana matatizo Ya Akili
Hayo yanatokea baada ya kushutumiwa na wataalam walugha za alama kwa kutafsiri ama kutoa ishara tofauti na kile kilichokuwa kikizungumzwa
Hata hivyo yeye mwenyewe alisisitiza kuwa aliumwa ghafla wakati akiwa kazini na kwamba yeye ni mtaalam mzuri wa lugha hizo za ishara kutokana na kuwa ndio kazi yake ambayo amekuwa akiifanya kwa muda mrefu sana na ndio ambayo imekuwa ikimuingizia kipato na kulisha familia yake pamoja na kusomesha watoto wake
miongoni mwa Viongozi waliotafsiriwa ndivyo sivyo na bwana huyu ni Rais wa marekani Barak Obama
Chama tawala cha African National Congress,ANC, amesema imekuwa ikimtumia Bwana Jantjie kama mkalimani wa lugha ya ishara katika matukio kadha siku za nyuma na hakuwahi kulalamikiwa kuhusiana na huduma yake, kwa upande wa ujuzi au maradhi yoyote.
Bwana Mandela alifariki dunia tarehe 5 Desemba mwaka huu akiwa na umri wa miaka 95 na kuzikwa Jumapili.