Mamlaka ya usalama wa safari za baharini nchini Australia imesema kuwa operesheni ya kuitafuta ndege ya shirika la Malaysia iliyotoweka imesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa na mawimbi makali baharini.
Taarifa zinasema kuwa upepo mkali pamoja na mvua kubwa inayonyesha katika eneo hilo ina maana kuwa ndege hazitoweza kupaa kwa usalama.
Mawimbi makali yameilazimisha meli ya jeshi la wanamaji wa Australia kuondoka katika eneo ambalo mabaki yanayodhaniwa kuwa ya ndege hiyo yalionekana hapo jana Jumatatu.
Wakati huo huo ndugu na jamaa wa abiria waliokuwemo katika ndege hiyo wameandamana katika jiji la Beijing huku wakionekana kuwa na hasira baada ya kupata ujumbe uliosema hakuna mtu aliyenusurika katika ajalo hiyo..