Baada ya kuweka historia kwa kuwa mwanamuziki aliyeuza zaidi copies nyingi katika wiki ya kwanza kwa kuuza copies milioni 3.38 za albamu yake, Adele bado hajui kwanini Wamerikani wamepata kichaa na albamu yake aliiambia TIME.
“Haieleweki kidogo, hata sitokei Marekani, labda wanadhani nahusiana na malkia, Wamarekani wanapenda sana familia ya kifalme” Pia alikubali kwamba haimuingii akilini jinsi watu maarufu wanavyopenda mitandao ya kijami alisema “It’s ridiculous that high-profile people have that much access to the public,” How am I supposed to write a real record if I’m waiting for half a million likes on a photo? That ain’t real.”
Pia alifunguka hafanyi muziki wa wasanii ambao wanakuwa vichaa kwa
umaarufu…
“Baadhi ya wasanii,jinsi wanavyozidi kuwa wakubwa , na ndivyo wanavyozidi kuharibu na ndivyo inavyowafanya wachukiwe zaidi, sijali hata kama unatengeneza albamu kali ,kama sikupendi,sinunui albamu yako,sitaki wimbo wako usikike kwenye nyumba yangu kama nadhania wewe ni bastard” alifunguka Adele.