Tuzo za AFRIMMA zimepangwa kufanyika Julai 26 2014 na siku ndo hizo zishakwisha ni kesho kutwa tu, na katika shamra shamra za tuzo hizo kutakuwa na matukio ya utangulizi , kutakuwa na pre-party itakayofanyika Dallas Texas Ijumaa 13 Juni 2014 ndani ya Nai Lounge.
Katika party hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii mbalimbali na alie midomoni mwa wengi ambae atatoa burudani ni mkali kutoka Jamaica the reggae supa star Demarco, Eddy Kenzo kutoka Uganda na msanii mpya kutoka Big A Entertainment Teddy-A.
Itafuatiwa na party ambayo itajumuisha washiriki wote huko Nigeria tarehe 21 Juni ndani ya Quilox Lounge katika Mtaa wa Ozumba Mbadiwe, kisiwa cha Victoria jijini Lagos.
Walioalikwa kuhudhuria tukio hili ni wasanii mbalimbali kutoka barani Afrika na wale wa Nigeria watakuwepo.