Wasanii wa filamu nchini wameonekana kuguswa sana na kifo cha Msanii mwenzao na Muongozaji Filamu Adam Kuambiana Aliyefariki ghafla kwa matatizo ya vidonda vya Tumbo
Adam Kuambiana Amezikwa Leo Juma Nne Katika Makaburi ya kinondoni Jijini Dar Es Salaam ikiwa ni wasia wakutaka azikwe Hapa Dar Es Salaam Pindi Atakapofariki
Pamoja Na Wasanii Wa filamu wengi kuhudhuria mazishi hayo pia kulikuwa na wasanii wengine kutoka katika fani tofauti tofauti pamoja na baadhi ya viongozi kutoka Serekali
Marehemu Adam Philip Kuambiana alizaliwa mwaka 1976 Ifunga Mkoani Iringa
Mungu Ailaze Roho Ya Marehemu Mahali pema Peponi
Amen
Picha kwa hisani ya Othman Michuzi