Polisi jijini New York nchini Marekani wameanza uchunguzi kubaini chanzo cha ajali ya treni ya abiria iliyoua watu wanne na kujeruhi wengine zaidi ya 60 Mamlaka za Usalama za nchi hiyo zimesema zitaanza uchunguzi wake kwa kumhoji dereva wa treni hiyo aliyenusurika katika ajali hiyo iliyotokea jana na kukichunguza pia kisanduku cheusi cha mawasiliano cha treni hiyo. Treni hiyo ilipata ajali majira ya asubuhi katika kituo cha Spuyten Duyvil, karibu na mji wa Bronx ikielekea kusini mwa mji wa Manhattan ikiwa na abiria 150, baada ya mabehewa manne mpaka matano ya treni hiyo kuacha njia kutokana na sababu ambazo bado hazijafahamika. Kwa mujibu wa mamlaka zinazohusika na masuala ya zimamoto na uokoaji katika mji huo,watu 11 kati ya 63 waliojeruhiwa katika ajali hiyo hali zao ni mbaya huku sita kati yao wakiwa mahututi