Esta Akothe stage name anatumia “Akothee” ni msanii kutoka 254 Nairobi nchini Kenya, msanii katika kuanza safari yake ya muziki amepitia changamoto mbalimbali mpaka hapa alipo, msanii huyu kabla ya kuanza kufanya muziki alikuwa akiuza sabuni akitembeza mkononi, Kibongo bongo tunawaita wamachinga, pia alishakuwa dereva tax.
Akothe ni msanii ambae anakipaji kikubwa sana cha kucheza, alikuwa akicheza sehemu mbalimbali ambapo wazungu walikuwa wakipenda alichokuwa akikifanya wakawa wanamtunza pesa nyingi.
Akothe alialikwa nchini Uholanzi kufanya show ambapo alipata dola 3,000, mwanzoni alikuwa akiendesha tax ambayo haikuwa nzuri sana baada ya hapo akanunua gari aina ya Noah ikiwa ni gari yake ya pili.
Kwa sasa anamafanikio makubwa sana, ameajiri watu zaidi ya 20 anawalipa mishahara na pia mafanikio mengine.
Katika hustle zake akakutana na Mtangazaji wa Citizen radio na Televisheni katika kipindi cha Mseto, William Tuva a.k.a Mzazi Tuva kama wengi wanavyomfahamu “Yani ni kama wamalaika alimleta Tuva katika maisha yangu, ambae ameamua kunisaidia baada ya kuona kuna kitu ndani yangu, kuna kipaji” alisema Akothe wakati akiongea na Tj na Jimmy Jay katika Dala Dala Beatz ya Magic FM.
Akaothe ana watoto watano lakini ukimuangalia huwezi kuamini kuwa ana watoto watano kwa sababu ana mwili mzuri sana.
Akizungumza Mzazi Tuva amesisitiza wasanii wa Afrika Mashariki kupendana na kupeleka muziki wetu mbali zaidi ili tuweze kufanikiwa zaidi ya hapa tulipo.
Akothe ametembea nchi nyingi duniani lakini kwa Tanzania hii ni mara ya kwanza kufika.
Kupitia Magic FM Magic Stick Akothe ametambulisha wimbo wake mpya unaoitwa “Katika” ni ngoma moja iliyochangamka na nzuri sana.
Wakati huo huo mkali kutoka kundi la Weusi, G Nako alitambulisha ngoma mbili, “Mavijana” feat Lord Eyez na “Chunga Unyumba” feat Nick Wapili.