Albamu ya repa anayeongoza kwa beef repa anayewakilisha Compton to death amepanga kuachia albamu yake inayoitwa Blood Money La Familia itatoka Septemba 16.
Project hiyo itakuwa na ngoma kama “Bigger than me” na “Or Nah” ambayo imeapnagwa kuwa project ya kwanza akiwa na Entertainment One Music baada ya kuachia albamu zake za mwanzo tano kupitia kampuni tofauti tofauti.
Game mwenyewe na mtayarishaji mkuu wa albamu hiyo akiwa na Cash Wack Jones na Stat Quo. Alan Grunblatt rais wa One Music anasema Game ni msanii asiye na mfano “Game anafanya muziki ambao watu wanaujali, natazama zaidi mbele kuwa na mahusiano ya muda mrefu na uhusiano utakaokuwa na matunda kati ya Cash Jones na eOne” alisema rais huyo.
Mwezi Juni tarehe 5 mwaka huu wa 2014 Hip Hop Dx iliripoti kwamba Game alisema wakati akipiga stories na radio ya Los Angeles Power 106 kwamba anabadilisha jina la albamu yake kutoka Blood Money La Familia na kuitwa “Year of the Wolves” mwezi uliopita tena akasema itaitwa jina lile lile la Blood Money La Familia, nadhani hili ndio jina la albamu ambayo itatoka mwezi Septemba tarehe 16 hatutegemei kama itabadilishwa jina…Good luck Game The Compton California rapper.