Muimbaji aliyewahi kushinda tuzo ya Grammy Lauryn Hill (pichani) amehukumiwa adhabu ya kifungo cha miezi mitatu jela kwa kushindwa kulipa kodi ya takriban dola milioni 1.
Mwanamuziki huyo mwenye umri wa miaka 37 aliyekuwa na kundi la Fugees pia amehukumiwa kifungo cha nyumbani cha miezi mitatu.
Wakati akitoa utetezi wake kwa jaji, Hill alifafanua kuwa siku zote alikuwa na nia ya kulipa kodi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa kipindi ambacho aliachana na biashara ya muziki.