Mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa nchini Kenya Raila Odinga, Fidel Odinga amefariki kifo cha ghafla siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili 4/1/2015 akiwa nyumbani. Kifo hicho kimewashtua watu maarufu nchini Kenya wakiwemo wanasiasa, wahubiri na mastaa wa burudani.
Watu wengi maarufu wametuma rambi rambi akiwemo msanii wa Bongo Flava kutoka nchini Tanzania almaarufu kama AY. Katika ujumbe wa AY alipost picha yake na Fidel Odinga ikiambatana na ujumbe aliondika #REST IN PEACE #FIDELODINGA.
Fidel alikutwa amekufa kwenye nyumba yake huko Karen mapema siku ya Jana Jumapili, na kilichosababisha kifo chake mpaka sasa hivi hakijafahamikia lakini mara ya mwisho alitoka out na marafiki marafiki zake wameshahojiwa na taarifa zitatoka ilikuwaje.
Familia ya Odinga imepanga kupumzisha au kuuzika mwili wa mpendwa wao siku ya Jumamosi 10/1/2015 katika eneo la Baba yake huko Bondo.
Fidel atakumbukwa kwa sababu alikuwa ni mtu aliyejichanganya na watu wa hali zote masikini, matajiri bila kujali alikuwa wa watu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Ambene Yesaya A.Y Atuma Salamu Za Rambi Rambi Kwa Familia Ya Raila Odinga
Related Posts
-
-
Pope Francis Kujiuzulu Kama Ilivyotokea Kwa Pope Benedict (XV1)
-
Mariam Ibrahim Mwanamke Aliyewahi Kuhukumiwa Kifo Nchini Sudani, Apokelewa Italy Na Waziri Mkuu Wa Nchi Hiyo
-
Nyota wa BollyWood Sunjay Datt ahukumiwa miaka 5 Jela kwa kesi ya mwaka 2003
-
Watoto Wa Mandela Waanza Kugombea Mali Za Baba Yao
-
George Alexander Louis Ndio jina la Mwana Mfalme Wa Uingereza aliyezaliwa
-
Nigeria Yafanikiwa Kuangamiza Ebola