Mtoto wa waziri mkuu wa zamani wa nchini Kenya Raila Odinga, Fidel Odinga amefariki kifo cha ghafla siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili 4/1/2015 akiwa nyumbani. Kifo hicho kimewashtua watu maarufu nchini Kenya wakiwemo wanasiasa, wahubiri na mastaa wa burudani.
Watu wengi maarufu wametuma rambi rambi akiwemo msanii wa Bongo Flava kutoka nchini Tanzania almaarufu kama AY. Katika ujumbe wa AY alipost picha yake na Fidel Odinga ikiambatana na ujumbe aliondika #REST IN PEACE #FIDELODINGA.
Fidel alikutwa amekufa kwenye nyumba yake huko Karen mapema siku ya Jana Jumapili, na kilichosababisha kifo chake mpaka sasa hivi hakijafahamikia lakini mara ya mwisho alitoka out na marafiki marafiki zake wameshahojiwa na taarifa zitatoka ilikuwaje.
Familia ya Odinga imepanga kupumzisha au kuuzika mwili wa mpendwa wao siku ya Jumamosi 10/1/2015 katika eneo la Baba yake huko Bondo.
Fidel atakumbukwa kwa sababu alikuwa ni mtu aliyejichanganya na watu wa hali zote masikini, matajiri bila kujali alikuwa wa watu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
Ambene Yesaya A.Y Atuma Salamu Za Rambi Rambi Kwa Familia Ya Raila Odinga
Related Posts
-
-
Iggy Azalea Amshambulia Kwa Maneno Paparazi Amwambia Anatumaini Jamaa Anaumwa Ebola
-
Kwa Mara Ya Sita Dhamana Ya Bobby Shmurda Yakataliwa
-
Rihanna Ni Sababu Ya Rita Ora Kuishtaki Roc Nation
-
Mavazi Ya Watoto Wa Obama Sasha Na Malia Kichefchef, Hayana Heshima, Yakosolewa
-
Justin Bieber Chini Ya Ulinzi kwa Kuendesha Gari Akiwa Amelewa, Huku Akishindana Mbio Za Magari Zisizo Rasmi
-
Chinua Achebe Muandishi Nguli Wa Vitabu Duniani Afariki huku dunia bado ikimuhitaji