Askari mmoja wa kike Raia wa Kenya ‘Linda Okello’ amenusurika kupoteza kibarua chake kufuatia kivazi cha kubana alichokuwa amevaa wakati yupo kwenye majukumu ya kikazi kumchora sehemu kubwa ya maungo yake ikiwemo makalio kitendo kilichopelekea picha yake kusambaa kwa kasi kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook na Twitter.
Baada ya Taarifa pamoja na picha kuwafikia wakuu wake wa kazi, aliweza kuitwa na kamanda wa polisi wa kanda hiyo ‘James Mugeria’ na kupewa onyo kali juu ya mavazi yake ambayo yalionekana kuonyesha kielelezo kibaya katika jamii.
Hata hivyo Afisa huyo wa Forodha aliachiwa na kuendelea na majukumu yake kama kawaida baada ya kupewa agizo la kubadili mfumo mzima wa mavazi yake pindi awapo kazini. Picha ya afisa huyo wa forodha ilipigwa mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa kwenye majukumu ya kikazi na mwenzake eneo la Kiambu nchini Kenya.