
Polisi wa Florida walipiga picha na 50 cent katika jengo la mahakama mwezi uliopita.
Mwezi uliopita 50 cent alikuwa Palm Beach huko Florida kwa ajili ya kesi, wakati akitembea katika jengo hilo,repa huyo alipiga picha na mwanasheria wa muhanga aliyebakwa na polisi watatu waliokuwa eneo hilo.
Mkubwa mmoja wa Polisi wa eneo hilo la Palm Beach imeripotiwa aligundua kuhusu picha hizo wikiendi iliyoisha ndipo alipoongea nao na kuwaonya vikali askari hao.
Siku za nyuma pia mkali Ray J alishapiga picha na polisi nakupost na ilimletea matatizo askari huyo, kwa Marekani ni nom asana kupiga picha na sakari ukapost kwenye mitandao ya kijamii angalau ikiwa kwa ajili ya matumizi yako binafsi ukaweka ndani.
Wote waliohusika kwenye sehemu hiyo wamejiweka matatani kwa sababu wanakuwa hawajali wanachokuwa wanakifanya wanashau kama wako kazini na kuanza kupiga picha.
