Mastaa wanazidi kuachana tu baada ya kuripotiwa kuachana kwa Future Na Ciara na jinamizi hilo likiwa linanyatia ndoa ya Jay Z na Beyonce kutokana na stories kibao zilizotawala mitandao kote duniani kwamba mara Beyonce atafuta nyumba bila Jay Z kujua, mara Beyonce anamuongelea Jay Z kutokuwa mwaminifu kwenye ngoma zake hata ule ugomvi wa kwenye lifti ulitokea baada ya Jiga kutaka kwenda kwenye party nyingine baada ya Met Gala na hiyo party huko alikuwepo the bad gal Riri.
Story ni kwamba mkali Tyga na Blac Chyna wameripotiwa kuachana baada ya kudumu kwa mwaka mmoja, lakini Chyna yeye amekana taarifa za TMZ zimeeleza. Taarifa hiyo haijaeleza sababu ya wawili hawa kuachana lakini taarifa iansema kwamba Blac Chyna amekana na kwamba ameendelea kuweka vitu vyake vingi nyumbani.
Tyga alisimamia pool parties mbili siku za karibuni ikiwemo kusherekea maisha yake alikuwepo mwandishi na mwanmitindo Kylie Jenner, Black Chyna hakualikwa kwenye party yeyote kati ya hizi kitu ambacho lazima kitaleta maswali kwa watu na kudhania mmeachana na kuna sehemu ukiwepo lazima upande wako awepo.
Wawili hao ambao walipata mtoto wa kiume anayeitwa King Cairo miaka miwili iliyopita inaripotiwa walianza kuwa wapenzi mwaka 2011 na rasmi walivalishana pete mwaka 2012. Na ilisharipotiwa Blac Chyna alikuwa katika ugomvi na Lil Durk na Tyga mwenyewe.
Lil Durk kuna ngoma ambayo aliongea kitu kuhusu Blac Chyna alisema
“What do strippers swallow? Maliah, Blac Chyna, just don’t tell Tyga” na walikutana na Tyga studio, Tyga akamwambia badilisha hiyo line lakini Lil Durk hakubadilsha ndo maana Tgya alimmind Lil Durk.
Je inaweza ikawa ni sababu ya Tyga kumuacha Blac Chyna? Kwa sababu Lil alisema what strippers swallow? Kwamba Blac alishaswallow mmmmmh!! Kama Ray J kwa Kim Kardashian I hit it first ndo Knaye West achukie amuache Kim…Uzuri Kanye ameanza mahusiano Kim anajua kila kitu hata ile video ya Ray J na Kim K wakila uroda.